Winning entries could not be determined in this language pair.There were 15 entries submitted in this pair during the submission phase, 4 of which were selected by peers to advance to the finals round. Not enough votes were submitted by peers for a winning entry to be determined.Competition in this pair is now closed. |
Ni nani aliyetupa nyanya ya kwanza iliyoleta mapinduzi ya La Tomantina? Ukweli ni kwamba hakuna ajuaye. Huenda ulikuwa uasi dhidi ya Franco, au sherehe iliyokithiri mipaka. Kulingana na habari zinazoaminika zaidi kuhusu kisa hicho, katika wakati wa sherehe ya Los Gigantes mnamo mwaka 1945 (paredi ya karatasi kubwa ya mâché puppet), wenyeji walikuwa wakitarajia kuanzisha vurugu ili waweze kuonekana. Walikuwa kwenye mkokoteni wa mboga hapo karibu na hivyo wakaanza kurusha nyanya zilizoiva. Watu wasiokuwa na hatia waliokuwa wakitazama tukio hilo walijiingiza katika kitendo hicho hadi mwishowe kikawa ni kizaazaa cha kurushiana matunda mengi. Wale walioanzisha vurugu hilo walikuwa hawana budi ila kuwalipa wauzaji nyanya hizo, lakini huko kulipa hakukusitisha marudio ya vita vya kurushiana nyanya-na chanzo cha desturi mpya. Viongozi waliogopa kuenea kwa vurugu hilo, hivyo wakaweka sheria, kisha wakazilegeza, kisha baadaye wakapiga marufuku itikadi hiyo mnamo miaka ya 1950. Ulipofika mwaka wa 1951, wale wenyeji waliovunja sheria hiyo walifungwa jela hadi wananchi waliposhinikiza serikali kuwaachilia huru ndipo wakatolewa jela. Marufuku ya vurugu la nyanya iliyokuwa mashuhuri zaidi ni ile ya mwaka 1957 wakati watu wa mrengo wa nyanya walipoandaa mazishi ya mwigo ya nyanya yaliyojumuisha jeneza na vilevile msafara. Baada ya mwaka 1957, serikali ya mitaa iliamua kulegeza msimamo wao mkali, na kuweka sheria kadhaa na hatimaye kukubali itikadi hii ya kuchekesha. Hata ijapokuwa nyanya hujumuishwa sana katika itikadi hii, sherehe mbalimbali huadhimishwa kwa juma zima hadi kufikia kilele cha kushambuliana kwa nyanya. Hii huwa ni sherehe ya watawa wa Buñol, Bikira Maria, na Mtakatifu Louis Bertrand, paredi za barabarani, muziki, fataki katika mtindo wa Kihispaniola. Katika hali ya kujiandaa kwa kujitia nguvu kwa makabiliano hayo, mlo mzuri wa paella huandaliwa katika mkesha wa makabiliano hayo. Mlo huo huwa ni wali wa Valencia, samaki, rangi ya njano inayotiwa kwenye chakula, na mafuta ya mzeituni. Leo hii, tamasha hili lina mpangilio wa kiasi fulani. Waandaaji wamefikia kiwango cha kutafuta aina maalum ya nyanya ambazo si tamu kwa ajili ya tukio hili la kila mwaka. Shamra shamra huanza kama saa 4:00 asubuhi, huo ndio wakati ambao wahusika hupiga mbio kuchukua hemu iliyowekwa juu ya mlingoti unaoteleza. Watazamaji huwamwagia maji kwa kutumia bomba huku wakiimba na kucheza barabarani. Kengele ya kanisani inapopigwa mnamo saa sita mchana, malori makubwa yenye shehena za nyanya huingia mjini, huku kelele za "To-ma-te, to-ma-te!" hufikia kilele. Kisha, mizinga ya maji hupigwa, na tukio lenyewe likaanza. Hicho huwa ndicho kiashirii cha wale wahusika kuanza kusaga nyanya na kushambuliana kwazo. wahusika wengine ni warushaji wa nyanya kutoka mbali, wengine ni washambulizi wa nyanya wa karibu, na wengine huzirusha kutoka umbali wa wastani. Haijalishi mbinu yako ni gani, lakini wakati tamasha litakapokwisha utakuwa na mwonekano (na utahisi) tofauti. Takriban saa moja baadaye, wale washambulizi wa nyanya husalia wakicheza salsa kwenye bahari ya nyanya zilizosagwa kiasi kwamba huwezi kuzitambua ni nyanya. Kisha mzinga wa pili huashiria mwisho wa mashambulizi hayo. | Entry #15538 — Discuss 0 — Variant: Not specified Finalist
|
Nani aliyerusha nyanya hiyo ya kwanza ya kimatukio iliyoanzisha mapinduzi ya ''La Tomatina''? Ukweli ni kwamba hakuna anayejua. Labda yalikuwa maasi dhidi ya Franco, au sherehe ya barabarani iliyozidi mipaka. Kulingana na maelezo yaliyo maarufu zaidi juu ya tukio hilo, katika sherehe ya "Los Gigantes" ya mwaka elfu moja mia kenda na tano(gwaride la majigumegume makubwa zaidi yaliyotengenezwa kwa karatasi za gundi), wenyeji walinuia kuzua ghasia za barabarani ili kuteka fikra za hadhira. Walivamia rukwama ya mboga iliyokuwa karibu na wakaanza kurusha nyanya mbivu. Waliokuwa katika hamsini zao walitekwa hadi eneo likakua kuwa ghasia kubwa za matunda yaliyopeperuka. Ilibidi wachochezi kuwalipa wachuuzi wa nyanya, ingawa hayo hayakuzuia kutukia tena kwa vita zaidi vya nyanya na uzawa wa desturi mpya. Kwa kuchelea tukio kupanda kuwa kiwango kisichozuilika, utawala ulitunga, ukalegeza kisha ukarejesha mfululizo wa marufuku katika miaka ya elfu moja mia kenda na hamsini. Wenyeji waliokaidi sheria wakifungwa jela hadi umma ulipozua kilio wafunguliwe. Uchokozi maarufu zaidi kwa marufuku dhidi ya nyanya ulitokea mwaka wa elfu moja mia kenda hamsini na saba wakati ambapo waneneaji walifanya mazishi maskhara ya nyanya makamilifu yaliyokuwa hata na jeneza na maandamano. Baada ya mwaka wa 1957 , serikali ya mtaa iliamua kukubaliana na hali kama ilivyokuwa, kiwango fulani cha kanuni na kukubaliana na desturi hii ya ajabu. Ingawa nyanya huchukua sehemu ya msingi kabisa, juma la sherehe hufikia tamati kwa mapambano ya mwisho. Ni maadhimisho ya watakatifu walezi wa Kibunol, Bikira Maria na mtakatifu Louis Bertrand, gwaride za barabarani, muziki na fataki kwa sherehe zenye shangwe za mitindo ya Kihispania. Ili kujenga siha yako kwa rabsha ijayo, huandaliwa ‘paella’- wali murwa usiku kutangulia pigano, kujivunia mlo wa wali maarufu wa Kivalensia, dagaa zafarani na mafuta ya mizeituni. Wa leo, sherehe hii isiyozuilika ina kiwango fulani cha utaratibu. Waandaji wamepiga hatua hata kukuza aina spesheli ya nyanya zisizolika kwa niaba tu ya tukio hilo la kimwaka. Sherehe huanzia takriban saa nne asubuhi wakati ambapo washiriki hukimbia kunyakua kipande cha nyama iliyokaushwa ya paja la nguruwe kilichotundikwa kwenye kikingi kilicholoa mafuta. Watazamaji huwapiga wanyang’anyanaji kwa mifereji ya maji wakiimba na kucheza densi barabarani. Kengele ya kanisa ikigonga saa sita mchana, malori yaliyosheheni nyanya huingia mjini hali nyimbo za “To-ma-te, to-ma-te” zikifika kilele. Kisha kwa ufyatuaji wa kanoni za maji, sherehe kuu huanza. Hiyo huwa ni kibali cha kuvunja nyanya na kufanya shambulizi pande zote dhidi ya washiriki wengine. Warushaji nyanya wa kulenga mbali, walengaji karibu na walenga shabaha wa wastani. Bila kujalisha mbinu yako ni gani, kipindi kinapofika hatima, utaonekana na kujihisi ukiwa tofauti kabisa. Takriban nusu saa baadaye, warushaji kombora za nyanya wanaachwa kucheza salsa ya barabarani katika bahari lililoloana likiwa na machache yanayofanana na nyanya kupatikana huko. Ufyatuaji wa kanoni ya pili huashiria mwisho wa vita. | Entry #18107 — Discuss 0 — Variant: Not specified Finalist
|
Ni nani aliyetupa ile nyanya ya kwanza kabisa iliyoibua mapinduzi ya La Tomatina? Ukweli ni kwamba hakuna anayejua. Pengine ilikuwa ni uasi dhidi ya Franco, au ilikuwa ni kanivali iliyopoteza mwelekeo. Hadithi maarufu kwa mujibu wa walio wengi ni kuwa, wakati wa sherehe za Los Gigantes (msururu wa vikaragosi vilivyoundwa kwa karatasi), wenyeji walitaka kuanzisha purukushani ili kupata kutambuliwa. Ikatokea kuwa wapo jirani na mkokoteni wa mbogamboga na kuanza kutupa nyanya zilizokuwa zimepea. Watu wasiokuwa na hatia wakiangalia nao wakajumuika hadi ikawa vurumai ya nyanya hewani. Wachochezi walilazimika kuwalipa wauza nyanya, lakini hiyo haikuzuia mwanzo wa utamaduni mpya. Zikiogopa kukua kwa vurumai hizi, mamlaka zikaweka, kuruhusu, na baadae kurudisha amri za kupiga marufuku mnamo miaka ya 1950. Mwaka 1951, wenyeji waliokiuka amri hii walifungwa hadi pale kilio cha watu wengi kilipodai waachiwe huru. Ujuvi uliopata kuwa maarufu zaidi kuliko wote kwa marufuku za vurumai hizi za kutupa nyanya ni ule wa mwaka 1957 ambapo watetezi wa utamaduni huu walifanya mfano wa maombolezo wakiandamana kwa kubeba jeneza la nyanya. Baada ya mwaka 1957, serikali za mitaa zikaamua kukubali mapigo, zikaweka sheria kadhaa, na kuruhusu utamaduni huu wa kipuuzi kuendelea. Ingawa nyanya bado zinakuwa ndio kiungo kikuu, wiki moja ya sherehe huanza kabla ya vurumai ya mwisho. Ni sikukuu ya walezi watakatifu wa Buñol, Maria Bikira na mtakatifu Louis Bertrand, ikijumuisha maandamano mitaani, muziki na fataki kwa namna ya furaha kwa Wahispaniola. Kujijengea nguvu kwa ajili ya mpambano unaokuja, chakula cha "paella" kililiwa siku ya kuamkia mpambano wa mwisho, aina ya chakula maarufu kule Valencia kikiwa na wali, aina mbalimbali za samaki wa bahari, zafarani na mafuta ya mzeituni. Siku hizi, sherehe hizi zisizopendwa zina aina fulani ya kanuni. Waandaaji wamefika mbali hadi kufikia kupanda nyanya ambazo hazina ladha kwa ajili tu ya tukio hili la kila mwaka. Shamrashamra huanza nyakati za saa nne asubuhi ambapo washiriki hukimbia kuinyakua hemu iliyoangikwa kwenye mlingoti uliopakwa grisi. Watazamaji huwamwagia maji washiriki huku wakiimba na kucheza mitaani. Kengele ya kanisa ikigongwa kuashiria saa sita mchana, malori yaliyojaa nyanya huingia mjini, wakati sauti za "To-ma-te, to-ma-te!"hufikia kileleni. Halafu, pindi mzinga wa maji unapopigwa, tukio kuu huwa linaanza. Hii ndio ruhusa ya kuponda na kutupa nyanya baina ya washiriki. Kuna wale wakirusha nyanya tokea mbali, wauaji wa karibu, na mapigo ya masafa ya kati. Kwa mbinu yoyote ile utakayotumia, utakaonekana (na kujisikia) tofauti kabisa. Baada ya muda wa saa moja hivi, watupiana mabomu waliolowa nyanya huachwa kucheza salsa kwenye bahari ya ujiuji kukiwa hakuna dalili ya kitu kinachofanana na nyanya kilichosalia. Mzinga wa pili ukipigwa unaashiria mwisho wa mpambano. | Entry #17323 — Discuss 0 — Variant: Not specified Finalist
|
Ni nani aliyetupa nyanya ya kwanza iliyoanzisha mapinduzi ya Kitomatina? Ukweli ni kwamba hakuna anayejua. Labda ilikuwa ni uasi wa kupinga Ufaransa, au mdundiko uliopitiliza mpaka ukaharibu. Kufuatana na hadithi inayojulikana zaidi, wakati wa sherehe za mwaka 1945 za Los Gigantes (maandamano ya vikaragosi vikubwa vya makaratasi), wenyeji walikuwa wanatafuta namna ya kuanzisha ugomvi ili watambulike. Wakakuta mahali kuna mkokoteni wenye matunda wakaanza kurusha nyanya mbivu. Watazamaji wasiohusika nao wakaingia mpaka hali ikawa kama mtafaruku wa matunda yanayoruka. Ilibidi walioanzisha vurugu kuwalipa wauza nyanya, lakini hilo halikuzuia kutokea kwa mapambano mengine ya nyanya - na mwanzo wa utamaduni mpya. Kwa kuhofia kuongezeka kwa fujo zisizozuilika, uongozi ulitunga sheria, kuzilegeza, na kurudisha tena mlolongo wa makatazo kwenye miaka ya 1950. Mwaka 1951, wenyeji waliokuwa wakihalifu sheria walikuwa wanafungwa mpaka umma ulipoanza kulalamika ili waachiwe. Upinzani mkubwa wa wazi juu ya kukatazwa vita ya nyanya ulitokea mwaka 1957 wakati wapendekezaji walipokuwa na mazishi bandia ya nyanya wakiwa na jeneza na maandamano kabisa. Baada ya mwaka 1957, serikali ya jimbo iliamua kuachana na upingaji, ikaweka sheria chache, na kukubaliana na utamaduni huu mpya wa kichizi. Ingawa nyanya ndiyo hujulikana zaidi, lakini sherehe za wiki nzima ndizo huishia na mpambano wa mwisho. Ni sherehe za watakatifu walinzi wa Buñol, Bikira Maria na Mt. Louis Bertrand, kukiwa na mdundiko mitaani, muziki na fataki kwa mtindo wa kufurahisha wa Kispaniola. Ili kujijengea uwezo wa mpambano unaokuja, chakula maalumu cha Kivalensia kiitwacho paella chenye wali, mazao ya baharini, na mafuta ya mzaituni. Kwa sasa, sherehe hizo zisizozuiwa zina kiwango fulani cha mpangilio. Waandaji wamekwenda mbali kiasi cha kupanda aina maalumu ya nyanya zisizokuwa na ladha nzuri ambazo ni maalumu kwa tukio hili la kila mwaka. Sherehe huanza kwenye kama saa 4 asubuhi wakati washiriki wanapokimbilia kuwahi kuchukua kipande cha nyama ya nguruwe iliyowekwa juu ya nguzo inayoteleza. Watazamaji huwalowanisha kwa maji ya kwenye mpira huku wakiimba na kucheza mtaani. Wakati kengele ya kanisa ikigongwa kuashiria saa sita mchana, magari yaliyosheheni nyanya huingia mjini, wakati huohuo nderemo za "Nya-nya, nya - nya" hufikia upeo. Halafu, kufuatia kupigwa kwa kishindo cha mzinga wa maji, tukio kuu huanza. Hicho ndio huwa kiashirio cha kuanza kusaga na kurusha nyanya katika mpambano halisi dhidi ya washiriki wengine. Warusha nyanya kwa mbali, wauaji wa karibu na walenga shabaha wa masafa ya kati. Kwa mtindo wowote ule, mpaka shughuli ikiisha, utaonekana (na kujisikia) tofauti sana. Baada ya kama saa moja baadaye, wapambanaji waliojaa nyanya huachwa kucheza salsa ya mtaani kwenye bahari ya utelezi kukiwa kumebakia dalili ndogo sana ya kitu kinachofanana na nyanya. Mzinga wa maji wa pili huashiria mwisho wa vita hiyo. | Entry #18665 — Discuss 0 — Variant: Not specified Finalist
|
Ni nani alikuwa wa kwanza kurusha nyanya zilizoanzisha mageuzi ya La Tomatina? Ukweli ni kwamba, hakuna ajuaye. Labda ni uasi uliompinga Franco, au nduli liloshidwa kuthibitiwa. Kwa mujibu wa hadithi iliyopata umaarufu zaidi, wakati wa tamasha ya 1945 ya Los Gigantes (waridhe kubwa la vibonzo vilivyoundwa kutokana na karasi zilizoloweshwa maji), wenyeji walikusudia kufanya fujo ili waweze kutambuliwa. Walipata rukwama yenye nyanya mbivu karibu nao na kuanza kuzirusha. Watazamaji waliokuwepo walijipata ndani ya fujo hizo na hali ikazorota na kuwa mrusho mkali wa nyanya. Wachunguzi waliwafidia wauzaji wa nyanya, lakini hilo halikuzuia marudio ya vita zaidi vya nyanya – na mwanzo wa utamaduni mpya. Kutokana na uoga wa kuongezeka kwa hali ya kutotii sheria, mamlika ziliweka, zikaondoa na kurudisha tena misururu ya marufuku katika miaka 1950. Mnamo mwaka wa 1951, wenyeji waliokiuka sheria walifungwa jela mpaka umma ukalilia kuwachiliwa kwao. Ukiukaji maarufu zaidi dhidi ya marufuku ya nyanya ulifanyika mwaka wa 1957 wakati waungaji mkono walifanya sarakasi ya mazishi bandia wakiwa na jeneza na matembezi. Baada ya 1957, serikali ya mtaa iliamua kuhepa hepa, ikaweka kanuni chache, na ikakubali utamaduni huu usioleweka. Ingawa nyanya zinaangaziwa zaidi, juma moja la tamasha mbali mbali humalizia kwa pambano la mwisho. Ni sherehe za watakatifu wa Buñol's patron, bikira Maria na Mtakatifu Louis Bertrand, pamoja na mawaridhe ya barabarani, muziki, na fataki za mtindo wa furaha wa Kihispania. Ili kujenga nguvu zako kwa maandalizi ya pambano linalotarajiwa, mlo wa mwaka wa paella huliwa siku moja kabla ya makabiliano, ili kuonyesha chakula cha utamaduni wa Valencia ambacho ni mchanganyiko wa wali, vyakula vya majini, saffron, na mafuta ya mizeituni. Siku hizi, tamasha hili hili lisilokuwa na vikwazo lina utaratibu fulani. Waandalizi wameendelea kiasi kwamba wamelima aina ya nyanya fulani ambazo haziliwi kwa minajili ya tukio hili la kila mwaka. Hekaheka huanza mwendo wa saa nne asubuhi ambapo washiriki huanza hushindana kukimbia kuchukua nyama ya nguruwe ambayo imewekwa kwenye mlingoti uliopakwa grisi. Watazamaji hunyunyiza maji kwa kutumia mipira ya maji huku wakiimba na kucheza kwenye barabara. Kengele ya kanisa inapogonga saa sita adhuhuri, magari makubwa yaliyojaa nyanya huingia mjini, huku kelele "To-ma-te, to-ma-te!" zikifika kileleni. Halafu, kwa tufyatua maji kwa kutumia kanoni, tukio kamili huanza. Hiki ndicho kibali cha mwanzo wa kufinya na kurushiana nyanya katika mashambulizi baina ya washiriki. Warushaji nyanya wa masafa marefu, wauajia wa wazi, warushaji wa masafa ya wastani. Mbinu yoyote utumiayo, kufikia mwisho, utaonekana (na kujihisi) tofauti kabisa. Takribani saa moja baadaye, washambuliaji walioloa nyanya wanaachwa wakicheza kwenye barabara iliyojaa vitu visivyoweza kutambulika kama awali vilikuwa nyanya. Ufyatuaji wa pili wa maji kwa kutumia kanoni hukamilisha pambano. | Entry #18892 — Discuss 0 — Variant: Not specified
|
Aliyeirusha ile nyanya ya kwanza iliyoanzisha mapinduzi ya Tomatina ni nani?hakika hakuna ajuaye.Huenda ulikuwa ni uasi dhidi ya Franco, au tamasha lililoshindikana kudhibitiwa .Kwa mujibu wa hadithi maarufu ya hivi sasa, wakati wa tamasha la mwaka 1945 la Los Gigantes (Karatasi kubwa la mâché la kuchezea gwaride wanasesere), wenyeji walitazamia kufanya ugomvi ili waweze kutiliwa maanani.Walipata kuwa jirani na toroli la kuuzia mbogamboga na wakaanza kurusha nyanya mbivu.Watazamaji wasio na hatia walishirikishwa mpaka ikawa tafrani kubwa ya matunda yapaayo.Na wachochezi walipaswa kuwalipa wachuuzi wa nyanya,lakini hilo halikusitisha kuibuka kwa mapigano zaidi ya nyanya-na hatimye kuzaliwa kwa utamaduni mpya. Ikihofia hali tete,mamlaka ililegeza, na halafu ikaweka mfululizo wa marufuku katika miaka ya 1950.Mnamo waka 1951, wenyeji waliokaidi sheria walifungwa jela mpaka umma ulipopiga kelele kutaka waachiwe.Ujasiri mkubwa wa kupinga marufuku ya nyanya ulitokea mwaka 1957 ambapo waungaji mkono waliigiza msiba na kufanya mazishi ya nyanya zikiwa jenezani.Baada ya mwaka 1957,serikali ya mtaa iliamua, kutunga taratibu chache,na kuuridhia utamaduni wa kiwendawazimu. Ingawa nyanya huchukua nafasi pekee, juma la sherehe hupelekea kilele cha fainali.Ni kusherehekea walezi watakatifu wa Buñol, Bikira Maria na Mtakatifu Louis Bertrand kwa matembezi mitaani,muziki na mafataki kwa mtindo wa Kihispania kwa shangwe.ili kujenga nguvu kwa ajili ya pambano lijalo,chakula murua paella huandaliwa wakati wa kilele cha pambano,wakionesha chakula cha Kivalensia chenye wali,vyakula vya baharini,safroni na mafuta ya zeituni. Leo, tamasha hili lisilo na kizingiti lina baadhi ya vigezo .Waandaaji wamekwenda mbali zaidi na kulima aina maalumu ya nyanya zisizovutia mahususi kwa tukio la mwisho wa mwaka.Sherehe zaanza kama saa nne za asubuhi ambapo washiriki hushindania kupata kipande cha nyama nyembamba ya nguruwe kutoka begani kilichowekwa juu ya nguzo yenye grisi.Watazamaji huwamwagia maji kwa mpira wagombaniaji huku wakiimba na kucheza mitaani.Kengele ya kanisani ya adhuhuri inapolia, malori yaliyosheheni nyanya hukatiza mjini,na ambapo ukelele wa ''To-ma-te, to-ma-te!'' hufikia mshindo wa juu. Baada ya maji kunyunyizwa, tukio nyeti huanza.Hiyo ni taa ya kijani kuashiria kuponda nyanya na kufanya mashambulizi dhidi ya washiriki wenzenu. Warusha nyanya wa masafa marefu,wauaji wa papo kwa papo,wa masafa ya kati.Mbinu yako yoyote ile,inapofikia kikomo, utaonekana(na kujihisi) tofauti sana. Karibia saa nzima kwa baadaye,wapiga mabomu waliotapakaa nyanya huachwa wacheze katika bahari ya muziki maridhawa wa salsa mitaani wakati kidogo kikibakia kufanana na nyanya kuja kupatikana. Kunyunyizwa kwa maji mara ya pili huashiria kumalizika kwa pambano. | Entry #16730 — Discuss 0 — Variant: Tanzanian
|
Nani ndiye mtu wa kwanza kurusha nyanya iliyoibua mchezo wa kutupiana nyanya uitwao La Tomatina? Hakika hakuna ajuaye. Labda ilikuwa ni kitendo cha kuonesha uasi dhidi ya Franko, au ni furaha iliyopindukia katika shamrashamra fulani. Kwa mujibu wa moja kati ya masimulizi mengi, wakati wa shamrashamra za Los Gigantes (maandamano makubwa ya watu waliojivika vinyago usoni), wenyeji walikuwa wanatafuta namna ya kujidai wanapigana kusudi watu wengi wawaangalie. Kwa bahati jirani palikuwa na mkokoteni wenye mbogamboga na hivyo kuanza kutupiana nyanya mbivu. Waliokuwa wakitazama tu maandamano yale nao polepole walijiunga kwenye mapambano mpaka pale hali ilipofikia kuwa ni vurumai kubwa ya matunda yaliyorushwa. Wale wenyeji walioanzisha mapigano walilazimika kuwalipa wauza nyanya, lakini jambo hilo halikuzuia kuibuka tena mapigano ya kutupiana nyanya—na mwanzo wa utamaduni mpya. Wakihofia mapigano kupitiliza, watawala waliyapiga marufuku, kuyaruhusu na kisha kuyazuia tena mapigano hayo katika miaka ya 1950. Mnamo mwaka 1951, watu wote waliokiuka marufuku hiyo walifungwa jela hadi pale nguvu ya umma ilipowafanya waachiliwe huru. Mfano mashuhuri wa nguvu ya umma ni ule wa mwaka 1957, pale wananchi walipoigiza msiba kamili kuomboleza kifo cha nyanya wakiwa na jeneza na msafara. Baada ya mwaka 1957, serikali iliamua kukumbatia utamaduni huu mpya, huku ikiweka kanuni chache. Japo kurushiana nyanya ndio shughuli kuu, juma zima la sherehe anuai huitangulia tafrani kuu. Ni maadhimisho ya watakatifu wanaotambuliwa mjini Buñol, yaani Bikira Maria na Mt. Luisi Bertrand, kwa maandamano, nyimbo, na mafataki kama ilivyo desturi ya sherehe za Kihispania. Ili kupata nguvu tayari kwa pambano, washiriki hula pilau mahsusi usiku wa kuamkia siku ya mapambano, mlo maalum wa watu wa Valensia wenye mchele, samaki, binzari na mafuta ya mizeituni. Hivi sasa, kanuni chache zinaongoza sherehe hizi huria. Kwa mfano waandaaji hulima aina fulani ya nyanya zisizolika mahsusi kwa sherehe hizi za kila mwaka. Sherehe huanza takriban saa nne kamili asubuhi pale ambapo washiriki hushindana kunyakua pande la nyama lililo kwenye nguzo inayoteleza. Hali wakiimba na kucheza mitaani, watazamaji huwamwagia maji washiriki hao. Pale kengele za kanisani zinapolia muda wa mchana, magari yaliyosheheni nyanya hufika mjini, ambapo kelele za kushangilia "To-ma-te, to-ma-te!" hufikia kilele. Kisha, tukio kuu huzinduliwa kwa kupiga mzinga unaorusha maji. Hiyo ndio alama ya kuruhusu kukamua na kurusha nyanya dhidi ya washiriki wengine. Mashambulizi ya masafa ya mbali, ya kuwapiga walio karibu kabisa, na yale ya masafa ya kati. Mbinu yoyote utakayoitumia, utaonekana (na kujihisi) uko tofauti kabisa mwishoni mwa mapambano. Takriban lisaa lizima baadaye, wapiganaji waliolowa nyanya bado hurushiana rojo la nyanya mtaani huku kukiwa na nyanya chache zilizosalimika. Mzinga wa pili hupigwa kuashiria mwisho wa mapambano. | Entry #18028 — Discuss 0 — Variant: Tanzanian
|
Hatma ilikuwa ya nani ambaye alitupa nyanya ambalo lilianzisha mapinduzi ya La Tomatina? Ukweli ni kuwa hakuna anayejua. Labda ilikuwa uasi dhidi ya Franco, ama sherehe ya maonyesho iliyoshindwa kudhibitiwa. Kulingana na maelezo maarufu zaidi ya hadithi hiyo, wakati wa sherehe ya Los Gigantes mwaka wa 1945 ( Jagina la karatasi linalopitishwa kwenye gwaride), wenyeji walikuwa wanaangalia ili waanzishe rabsha ndiposa waweze kusikizwa. Ilitendeka pale ambapo rukwama ya mboga iliyopatikana pale na wakaanza kutupa nyanya zilizoiva. Watazamaji ambao hawakuwa na hatia pia wakatupa nyanya hadi pahali hapo pakawa pahali pakubwa pa kunyemelewa na kurushiwa matunda. Iliwabidi wachunguzi kuwalipa wachuuza nyanya, lakini hiyo haikusimamisha marudio ya visa vya vita vya nyanya - na hapo pakatokea uzawa wa tamaduni mpya. Kutoka na uoga wa visa hivi kuzidi, wenye mamlaka walitunga, wakatulia halafu wakarudisha marufuku kadhaa wakati wa miaka ya hamsini. Mwaka wa 1951, wenyeji ambao walivunja sheria walifungwa jela hadi kukawa na vilio vya umma ambavya vilisababishwa kuwachiliwa kwao. Mojawapo ya kiburi kuu kwa marufuku ya nyanya ilitendeka mwaka wa 1957 wakati waunga mkono walifanya mazishi kamili ya nyanya kikejeli pamoja na sanduku la maiti na maandamano. Baada ya mwaka wa 1957, Serikali ya mji iliamua kuafikiana na kipigo walichokipata, ikaweka sheria chache na kukubali tamaduni hiyo yenye kukosa mantiki. Ingawaje nyanya huchukua sehemu kuu, wiki nzima ya sherehe huelekezwa kwenye tukio la mwisho. Ni sherehe ya watakatifu wa Bunol Patron, Bikira Maria na mtakatifu Louis Bertrand, pamoja na gwaride kwenye mitaa, muziki, na milipuko ya Baruti kwenye mitindo ya kiispania. Ilikuwa na nguvu wakati wa rabsha, wali wa kivalencia unaliwa usiku wa kuamkia vita hivyo, inayoonyesha vyakula vinavyotoka Valencia pamoja na: Wali, vyakula vya bahari, kiungo cha saffron na mafuta ya mizeituni. Leo hii, sherehe hii ina kipimo fulani katika mwelekeo wake, waanzilishi wameenda ndani kabisa katika kutafuta nyanya ambazo haziwezi lika kutumika katika tukio hilo la kila mwaka. Sherehe zinaanza saa nne, wakati washiriki wanapishana ili kuchukua kitafunio aina ya "Ham" juu kwenye mti unaoteleza. Watazamaji huwamwagia wang'ang'anaji hawa maji wakiimba na kucheza kwenye mitaa. Wakati kengele za kanisa hugongwa mchana, malori yaliojazwa nyanya huingia mjini, huku watu wakishangilia " Nyanya, nyanya!" sauti zikizidi kuongezeka. Halafu, kwa kutumia bunduki ya maji, tukio kuu huanza. Hiyo ni mwangaza wa kijani kibichi ikiashiria kupasua na kurusha nyanya pande zote dhidi ya washiriki wenzako. Warushaji nyanya wa masafa marefu, wauwaji wa kushtukia, na milipuko mbalimbali ya umbali wa kati. Kwa kutumia mbinu yako yoyote, wakati mtamaliza, utaonekana na kujihisi tofauti. Baada ya kama saa moja, walipuzi wa mabomu wa nyanya zilizolowa wanawachwa kuchezea kwenye bahari ya mitaa telezi densi ya salsa pamoja na chochote kidogo kifananacho nyanya kitakachopatikana. Mlipuko wa pili unaashiria hitimisho la vita. | Entry #17017 — Discuss 0 — Variant: Not specified
|
Ni nani aliyerusha nyanya ya kwanza lililoanza mapinduzi ya La Tomatina? Ukweli ni kwamba hakuna ajuaye. Labda lilikuwa maandamano ya anti-Franco au sherehe la hadhara lililovuka mpaka. Kulingana na hadithi iliyosambazwa zaidi, katika sherehe la Los Gigantes mnamo mwaka wa 1945, wenyeji walikuwa wanatafuta kuonekana kwa kuanzisha vita. Ikatokea kuwa kuna mkokoteni wa mboga karibu na hao majamaa wakaanza kurusha nyanya zilizoiva. Waliosimama karibu bila habari walipurwa, nao wakaingilia mzozano huo mpaka ikasababisha mahali pote ikawa ni mboga zikirushwa hewani. Waliochochea mzozo huo ikabidii walipe fidia kwa wachuuzi wa nyanya lakini hilo halikuzuia kurushiana nyanya. Na hapo kukazaliwa mtiindo mpya wakupurana na nyanya. Kuhofia kuwa kupurana na nyanya italeta vita na ghasia, polisi walikomesha, wakatuliza na baadaye wakakomesha tena, muda kwa muda tendo hili la kupurana mnamo wa mwaka 1950. Mwaka uliofuatia wa 1951, wenyeji waliopuuza sheria hiyo walitiwa kizimbani mpaka kilio cha wananchi kuwaachilia kikaskika kila mahali. Upinzani wa sheria hiyo ilifika kileleni pale wananchi waliiga mazishi ya nyanya na wakafuatana kwa msafara mkubwa mnamo wa mwaka 1957. Baada ya hapo, viongozi wa eneo hilo wakalazimika kutuliza sheria hiyo kwa kuweka masharti kidogo tu na kuidhinisha mtindo huo uendelee. Ingawa nyanya ilichukuwa jukwa la kati, wiki kabla hapo ilitanguliwa na sherehe ya aina mbalimbali. Ilikuwa kufurahia wafu watakatifu wa Buñol, Mama Maria na St. Louis Bertrand iliyoenda sambamba na misafara mitaani, muziki na mlipuko wa mataa kwa mtindo wa sherehe ya Waspania. Katika kujenga nguvu kabla mpurano, mapochopocho ya pilau huandaliwa jioni kabla, inayoangaza aina tofauti ya mlo wa wali wa Valencia, aina kadha wa mlo wa baharini, saffron na mafuta ya zaituni. Leo, sherehe hii imepata kiwango cha uadilifu. Waandalizi wamejizatiti mpaka wakapanda nyanya zisizolika bali tu zimepandwa kwa sherehe hii ya siku moja mwakani. Shughuli huanza kama saa nne asubuhi ambapo wahudhuria hukimbia katika mashindano ya kuchukua kiweo toka mkuki wa kuteleza. Watazamaji huwamwagilia maji wanariadha hao huku wakiimba na kucheza ngoma. Wakati kengele la kanisa linapogonga kuashiria jua utosini, malori yaliyobeba nyanya huingia mjini, huku watu hupiga mayowe wakisema "NYa-nya, Nya-nya" mpaka kelele kufika kileleni. Kisha, kwa kulipua kombora la mfereji mkubwa wa maji, sherehe hiyo huanza. Hilo ndo ishara la kupurana na kulengana na nyanya kwa yeyote yule aliyekaribu na amehudhuria hoja hilo. Walengaji wa mbali, wakaribu na wale waliyo kati yao. Kwa njia yeyote ile ya upuraji, hoja hili linapomalizika, utafanana na utajihisi tofauti. Baada ya saa zima hivi, walionyunyiziwa rojo la nyanya huachwa kucheza katika bahari la rojo katika densi ambayo huwezi kuona chochote kinachofanana na nyanya nzima. Mlipuko wa pili kutoka kombora huidhinisha mwisho wa vita hivi. | Entry #16741 — Discuss 0 — Variant: Kenyan
|
Ni nani aliye tupa nyanya ya kwanza ambayo ilianzisha mapinduzi ya La Tomatina? Ukweli ni kwamba hakuna anayejua. Labda ilikuwa ni mapinduzi kushindana na Wafaransa, ama ilikuwa ni sherehe ambayo iliyosambaratika. Kulingana na taarifa iliyoenea zaidi, sherehe ya 1945 ya Los Gigantes (maandamano makubwa ya karatasi za kuunda), wakazi wa huko walinuia kufanya ghasia ili wapate kusikizwa. Walipatana na mkokoteni uliokuwa umebeba mboga na wakaanza kutupa nyanya mbivu. Watazamaji ambao hawakuwa na hatia yoyote walilazamika kuhusika hadi kukatokea fujo ya matunda kupurushwa kila mahali. Walioanzisha ghasia hawakuwa na budi kuwalipa wauzaji wa nyanya lakini hiyo haikusimamisha vita vya nyanya-na kuzaliwa kwa desturi mpya. Katika mwongo wa 1950, ili kuepukana na ghasia na fujo zaidi, serikali walikataza, wakageuza marufuku, kasha wakapiga marufuku tena desturi hiyo. Katika mwaka wa 1951, wakazi wa mtaa huu ambao walikiuka sheria hiyo walifungwa jela hadi watu wakadai kufunguliwa kwao. Ufidhuli maarufu zaidi ulifanyika mwaka wa 1957 ambapo wapinzani walifanya mazishi ya kuigiza yaliyokamilishwa na sanduku la maiti na maandamano ya watu. Kutoka 1957, serikali ya eneo hilo iliamua kufuata mkondo, waliweka amri chache na wakukubali mila hiyo ya kushangaza. Hata kama, nyanya ndio zinazovutia zaidi, kuna wiki moja ya sherehe hadi onyesho maalum la mwisho. Huu huwa ni wakati wa kusherehekea watakatifu marehemu wa nchi ya Bunol, mtakatifu Maria na Mtakatifu marehemu Louis Bertrand yenye maandamano ya njiani, muziki na fataki kulingana na desturi ya shangwe ya Uhispania. Ili kuongeza nguvu kabla ya ghasia zinazotarajiwa, chajio ambacho ni onyesho la wali wa Kivalensia, chakula cha baharini, zafarani na halzeti huandaliwa usiku wa kuamkia vita. Siku hizi, sherehe hii isiyo na vizuizi ina mpangilio fulani. Wasimamizi hupanda nyanya ambazo haziwezilika kwa manufaa tu ya sikukuu hii. Sherehe huanza saa nne za asubuhi ambapo wahusikaji hukimbia kunyakua kiweo ambacho huwa kimethibitishwa juu ya ufito wenye mafuta. Watazamaji hutupia maji wanaohusika katika kunyakua kiweo huku wakiimba na kucheza ngoma kwenye njia. Kengele ya kanisa inapopiga saa sita za mchana, malori yaliyojazwa nyanya huingia mjini watu wakipaza sauti wakiimba “To-ma-te, to-ma-te!” Mzinga wa maji unapoachiliwa, tukio maalum linaanza. Hii ndiyo ishara kwa wahusika kuanza kushambuliana katika msongano wa kuponda na kutupiana nyanya. Halaiki hutupiana nyanya kwa umbali, wengine kwa karibu na wengine kwa karibu zaidi. Haijalishi ustadi utakao tumia, wakati tukio hili linaisha utafanana na kuhisi tofauti sana. Saa moja baada ya shani, watu waliopakana nyanya wanawachwa kucheza kwenye njia iliyojaa unyevu wa nyanya zilizopondwa, bila hata ya nyanya moja kupatikana. Mzinga wa pili unapoachiliwa, huwa ni ishara kwamba vita vimefikia kikomo. | Entry #19859 — Discuss 0 — Variant: Kenyan
|
Ni nani aliyerusha ile nyanya jaliwa iliyoanza mapinduzi ya 'La Tamatina'? Ukweli ni kwamba hakuna anayejua. Huenda ikawa ni uasi dhidi ya Franco, au kanivali ambayo haingedhibitika. Kulingana na aina nyingi maarufu za hadithi hiyo, wakati wa sherehe ya 1945 ya 'Los Gigantes' (maonyesho ya karatasi kubwa sana, 'mâché puppet' ), watu walitaka kuzua mzozo ili kujulikana. Ilifanyika katika rukwama ya mboga iliyokuwa karibu na kuanza kurushiana nyanya zilizoiva. Watazamaji wasiokuwa na hatia walihusika mpaka mandhari ikaweza kuwa ghasia kubwa la tunda kuruka. Wachochezi walilazimika kuwalipa wachuuzu wa nyanya, lakini hilo halikumaliza kutokea kwa vita zaidi vya nyanya—na kuzaliwa kwa utamaduni mpya. Kwa kuogopa ueneaji mtukutu, Viongozi waliingililia kati, wakapunguza, na wakaamrisha mfuatano wa kupiga marufuku katika miaka ya 1950. Katika 1951, watu wasiofuata sheria walifungwa mpaka raia wakawezesha kuachiliwa kwao. Kuthubutu maarufu kwa kupiga nyanya marufuku, kulitokea 1957 wakati wapendekezaji waliweka mazishi ya mzaha ya nyanya wakiwa na jeneza na maandamano kamilifu. Baada ya 1957, serikali ya mtaa iliamua kufuata mkondo, ikaweka amri chache, na kukubaliana na utamaduni pumbavu. Ingawa nyanya huchukua mandhari ya kati, wiki ya sherehe hupelekea hadi kufungwa kwa mwisho. Ni sherehe ya watakatifu walezi wa Bunoli, Bikira Mariamu na Mtk. Louis Bertrand, na gwaride za mtaani, muziki, na fataki kwa mtindo wenye furaha wa Uispania. Ili kujenga nguvu zako kwa mzozano unaokaribia, chakula cha kisherehe hushirikiwa vita vinavyoendelea, kuonyesha chakula shupavu cha Kivalenzia cha wali, chakula cha baharini, zafarini, na mafuta ya zeituni. Leo, sherehe hii isiyosherehekewa ina mpangilio fulani. Wapangaji wameendelea mpaka wakaweza kukuza namna spesheli ya nyanya isiyo na ladha kwa tukio tu la mwaka. Sherehe huanza hapo saa nne asubuhi wahusika wanapokimbia kuchukua hemu iliyokaziwa juu ya nguzo telezi. Watazamaji huwamwagilia maji wanaong'ang'ania huku wakiimba na kucheza mitaani. Wakati kengele la Kanisa huashiria saa sita, Lori zinazobeba nyanya huingia mjini huku mkarara wa "To-ma-te, to-ma-te!" ukipaa juu. Basi, tukio halisi huanza kwa kufyatuliwa kwa mzinga wa maji. Hiyo ndiyo hupelekea kupondwa na kuzinduliwa kwa nyanya katika mapigo yote kwa wahusika wenyewe. Wanaorusha nyanya kutoka mbali, wauwaji maarufu, na milio wastani za kiopoo. Kwa mbinu yoyote ile, wakati wa kumaliza, utaangalia (na kuhisi) tofauti kabisa. Karibu lisaa moja baadaye, watupaji mabomu waliolowa katika nyanya huachwa ili kucheza katika ziwa la mdundo wa kufyonza wa mtaa pasipokubakia lolote linalofanana na nyanya. Mfyatuko wa pili wa mzinga huashiria mwisho wa vita. | Entry #21698 — Discuss 0 — Variant: Not specified
|
Ni nani aliyetupa nyanya ambayo iliyoanzisha mapinduzi ya La Tomatina? Ukweli nikua hakuna mtu anayejua. Labda ilikua ni uasi dhidhi ya Franco, au sherehe kubwa ambalo lilitoka nje ya mkono. Kulingana na taarifa mashuhuri la tukio, wakati wa sherehe ya 1945 mjini Los Gigantes (iliokua gwaride kubwa la kinyongo la karatasi), wenyeji walikuwa wakitazamia kuzua rabsha ili wapate kuonekana. Walikaribia na kujipata katika mkokoteni wa mboga uliokua karibu na kuanza kurusha nyanya zilizoiva. Watazamaji waliokua karibu wakajiunga kushiriki mpaka eneo mzima ilienea katika mvutano mkubwa wa matunda yakupepea. Iliwabidi waanzilishi kuwalipa wachuuzi hao wa nyanya, lakini hilo halikusababisha mwisho wa vita kama hivyo vya nyanya - nao ukawa mwanzo wa utamaduni mpya. Kwa uoga wa kupanda kwa ukaidi zaidi, mamlaka ilitunga, kuteremsha, na kisha kurejesha mfululizo wa marufuku katika miaka ya 1950. Katika mwaka wa 1951, Wenyeji ambao walikaidi amri walitiwa gerezani hadi kukawa na kilio kutoka kwa umma ili waachiliwe. Tukio la kwanza maarufu dhidi ya marufuku hio ya nyanya kilitokea mwaka 1957 wakati watetezi walifanya maskhara ya mazishi ya nyanya kamili na jeneza na maandamano. Baada ya 1957, serikali za mitaa iliamua kukwepa makonde na kuweka sheria chache kisha kukumbatia utamaduni huo. Ingawa nyanya huchukua hatua ya mbele, Wiki moja ya sherehe kuu hutawalia tukio kuu la mwisho. Ni sherehe ya watukufu wa Buñoli, Bikira Maria na Mtf. Louis Bertrand, kwa gwaride za mitaani, muziki, na miale za moto katika furaha ya mtindo wa Kihispania . Ilikujenga nguvu yako kwa rabsha iliyombele, chakula kitamu cha paella huhudumiwa usiku wa vita, manyesho makuu ya wali wa kivalensia,vyakula vya bahari, zafarani, na mafuta ya zeituni. Leo, sherehe hili kuu lina utaratibu wa kipimo. Waandalizi wamejitolea hadi kutayarisha na kupalilia aina maalum ya nyanya yasiokulika kwa ajili ya sherehe hili la mwaka. Sherehe zinaanza takriban saa 4 asubuhi hivi wakati washiriki watakimbia kunyakua paja la nyama lilioekwa juu ya fimbo refu. Watazamaji humwagilia wang'ang'aniaji maji huku wakiimba na kucheza barabarani. Wakati kengele la kanisa hugonga saa sita mchana, malori yalioezekwa nyanya huingia ndani ya mji, huku kelele za "to-ma-te! to-ma-te!" yakizidi kupanda. Basi, kwa kurushwa kwa kanuni la maji, tukio kuu huanza. Hilo huwa ndilo kiashiria cha mwanzo wa kusiaga na kurusha nyanya katika mashambulizi yote dhidi ya washiriki wengine. mitungi ya kurusha nyanya kwa umbali, ukabidhi wa ukaribu na kurusha shoti za wastani. Mbinu yoyote ile utakacho tumia, wakati utakapoisha, utakaa ( na kujisikia) tofauti kabisa. Karibu saa moja baadaye, wapiga bomu za nyanya walioloweka wanaachwa kucheza katika bahari ya mtindo wa salsa mithili wa nyanya yanayo patikana. Shoti la pili kutoka kanuni huashiria mwisho wa vita. | Entry #18994 — Discuss 0 — Variant: Kenyan
|
Ambao kutupwa kwamba kwanza ya tukio hilo, nyanya ambayo ilianza La Tomatina mapinduzi? Ukweli ni hakuna mtu anajua. Labda ni kupambana na Franco uasi, au Carnival kwamba got nje ya mkono. Kulingana na toleo maarufu wa hadithi, wakati wa sikukuu ya 1945 Los Gigantes (a kubwa karatasi Mache bandia gwaride), wenyeji walikuwa kuangalia kwa hatua rabsha kupata baadhi ya tahadhari. Wao kilichotokea juu ya mboga gari karibu na kuanza zakutupa muafaka nyanya. Watazamaji Innocent got kushiriki mpaka eneo ilienea katika melee mkubwa wa kuruka matunda. The instigators alikuwa na kulipa wachuuzi nyanya, lakini hawakuacha kujirudia zaidi nyanya mapambano-na kuzaliwa kwa utamaduni mpya. Waoga wa kupanda wakaidi, mamlaka ilipitishwa, walishirikiana, na kisha kurejeshwa mfululizo wa kusitisha katika Miaka ya 1950. Mwaka 1951, wananchi ambaye alipuuza sheria walikuwa jela hadi kilio kwa umma kuitwa kwa ajili ya kutolewa yao. effrontery maarufu kwa nyanya kusitisha kilichotokea mwaka 1957 wakati watetezi uliofanyika nyanya maskhara mazishi kamili na jeneza na maandamano. Baada ya 1957, serikali za mitaa aliamua unaendelea na kukwepa makonde, kuweka sheria chache katika mahali, na kuvutiwa wacky utamaduni. Ingawa nyanya kuchukua hatua ya kituo, katika wiki ya sikukuu kusababisha hadi showdown mwisho. Ni maadhimisho ya Buñol ya watu wa Mungu mlinzi, Bikira Maria na St Louis Bertrand, kwa gwaride mitaani, muziki, na fireworks katika furaha Kihispania mtindo. Kujenga yako nguvu kwa rabsha impending, paella Epic ni aliwahi katika usiku wa vita, showcasing iconic Valencian sahani ya mchele, dagaa, zafarani, na mafuta. Leo, sikukuu hii isiyokuwa na ina baadhi ya kipimo cha utaratibu. Waandaaji wamekwenda mbali kama kulima aina maalum ya nyanya unpalatable tu kwa ajili ya tukio la kila mwaka. Sikukuu kick off karibu 10:00 wakati washiriki mbio kunyakua ham fasta atop pole greasy. Watazamaji hose scramblers na maji wakati kuimba na kucheza katika mitaa. Wakati kanisa kengele mgomo saa sita mchana, malori packed na nyanya unaendelea ndani ya mji, wakati chants ya "Kwa-ma-te, to-ma-te!" kufikia crescendo. Basi, pamoja na kurusha ya kanuni maji, tukio kuu huanza. Hiyo ni mwanga kijani kwa ajili ya kusagwa na uzinduzi nyanya katika mashambulizi yote dhidi ya washiriki wenzake. Umbali mrefu nyanya lobbers, kiwango-tupu assassins, na kati mbalimbali shots ndoano. Chochote mbinu yako, na wakati ni juu, wewe kuangalia (na kujisikia) kabisa mbalimbali. Karibu saa baadaye, nyanya-kulowekwa bombers ni wa kushoto na kucheza katika bahari ya squishy mitaani salsa na kidogo kushoto yanafanana nyanya kwa kupatikana. kanuni pili risasi ishara ya mwisho wa vita. | Entry #18134 — Discuss 0 — Variant: Not specified
|
Ambao kutupwa kwamba kwanza ya tukio hilo, nyanya ambayo ilianza La Tomatina mapinduzi? Ukweli ni hakuna mtu anajua. Labda ni kupambana na Franco uasi, au Carnival kwamba got nje ya mkono. Kulingana na toleo maarufu wa hadithi, wakati wa sikukuu ya 1945 Los Gigantes (kubwa karatasi Mache bandia gwaride), wenyeji walikuwa kuangalia hatua rabsha kupata baadhi ya tahadhari. Wao kilichotokea juu ya mboga gari karibu na kuanza zakutupa nyanya zilizoiva. Watazamaji Innocent got kushiriki mpaka eneo ilienea katika melee mkubwa wa kuruka matunda. Instigators alikuwa na kulipa wachuuzi nyanya, lakini hakuwa na kuacha kujirudia nyanya mapambano-na zaidi ya kuzaliwa kwa utamaduni mpya. Waoga wa kupanda wakaidi, mamlaka iliyotungwa, walishirikiana, na kisha kurejeshwa mfululizo wa kusitisha katika miaka ya 1950. Mwaka 1951, wananchi ambaye alipuuza sheria walikuwa jela hadi kilio kwa umma kuitwa kwa ajili ya kutolewa yao. Effrontery maarufu kwa nyanya kusitisha kilichotokea mwaka 1957 wakati watetezi uliofanyika maskhara nyanya mazishi kamili na jeneza na maandamano. Baada ya 1957, serikali za mitaa aliamua kukwepa makonde, kuweka sheria chache katika mahali, na kuvutiwa utamaduni wacky. Ingawa nyanya kuchukua hatua ya kituo, katika wiki ya sikukuu kusababisha hadi showdown mwisho. Ni sherehe ya Buñol ya watu wa Mungu mlinzi, Bikira Maria na St Louis Bertrand, kwa gwaride mitaani, muziki, na fireworks katika furaha Kihispania mtindo. Kujenga nguvu yako kwa rabsha impending, paella Epic ni mjumbe katika usiku wa vita, showcasing iconic Valencian sahani ya mchele, dagaa, zafarani, na mafuta. Leo, sikukuu hii isiyokuwa na ina baadhi ya kipimo cha utaratibu. Waandaaji wamekwenda mbali kama kulima aina maalum ya nyanya unpalatable tu kwa ajili ya tukio la kila mwaka. Sikukuu kick off karibu 10 asubuhi wakati washiriki mashindano ya kunyakua ham fasta atop pole greasy. Watazamaji hose scramblers na maji wakati kuimba na kucheza katika mitaa. Wakati kengele kanisa mgomo saa sita mchana, malori packed na nyanya unaendelea ndani ya mji, wakati chants ya "Kwa-ma-te, to-ma-te!" kufikia crescendo. Basi, pamoja na kurusha ya kanuni maji, tukio kuu huanza. Hiyo ni mwanga kijani kwa ajili ya kusagwa na uzinduzi wa nyanya katika mashambulizi yote dhidi ya washiriki wenzake. Umbali mrefu nyanya lobbers, kiwango-tupu assassins, na aina mbalimbali kati ndoano shots. Chochote mbinu yako, na wakati ni juu, wewe kuangalia (na kujisikia) tofauti kabisa. Karibu saa baadaye, mabomu ya nyanya-kulowekwa ni wa kushoto na kucheza katika bahari ya squishy mitaani salsa na kushoto kidogo yanafanana nyanya kwa kupatikana. Pili kanuni risasi ishara ya mwisho wa vita. | Entry #17741 — Discuss 0 — Variant: Not specified
|
Nani ametupa lile nyanya la kwanza la majaliwa lililoanzisha mapinduzi ya "La Tomantina"? Ukweli ni kwamba hakuna anayejuwa. Labda ilikuwa uasi dhidi ya Ufaransa, ama kanivali iliosawijika. Kutokana na tafsiri ya karibu watu wote kuusu hadithi, wakati wa tamasha la mwaka 1945 la Los Gigantes (jitu la gwaride za karatasi), wenyeji walikua natafuta kufanya tamthilia la ghasia ili kuvutia macho. Walitukia juu ya mkokoteni za mboga za majani lililokua karibu na walianza kutupa kwa nguvu nyanya za kuiva. Watazamaji wasio na hatia waliusishwa hadi mandhari liligeuzwa mrundikano wa vurumai nyingi ya matunda inayoruka. Wachochezi walilazimika kulipa mara kwa mara wauza-nyanya, ila hiyo haikusimamisha marudilio ya ugomvi zaidi wa nyanya na kuzaliwa kwa desturi mpya. Kwa hofu la ongezeko tukutu, wakubwa waliifanya kuwa sheria, waliipunguza, na wakati ule walirejesha mahali pake mfululizo safu za amri ya kupiga marufuku mnamo miaka 1950. Mnamo mwaka 1951, wenyeji waliodharau sheria walifungwa jela hadi yowe ya umma uliomba ufunguliaji wao. Ujuvi mashuhuri kuliko yote ulitukia mwaka 1957 wakati watetezi walishika dhihaki kamili ya mazishi ya nyanya pamoja na jeneza na mfanyiko tendani. Baada ya mwaka 1957, serikali ya kienyeji liliamua kuenda na panchi, kuweka sheria kidogo hapo mahali, na lilipokea kwa moyo desturi ya upuuzi. Ingawa nyanya imechukua jukwaa iliolengwa, wiki mmoja ya sherehe ilifanya matayarisho ya onyesho la mwisho. Ni maadhimisho ya watakatifu walezi wa Bunol, Mtakatifu Maria na Mt. Louis Bertrand, pamoja na maonyesho ya mitaa, muziki, na fataki kwa mtindo wa kihispania ulio na furaha. Kwa kuongeza nguvu kwa ghasia inayokaribia, utendi wa paella anahudumiwa kabla ya mapambano, ikionyesha sahani ya wavalensi iliyochapiwa ya wali, vyakula vya baharini, zafarani, na mafuta ya zeituni. Leo, hii sherehe isio na vikwazo ina kiasi kya kipimo kya taratibu. Waandalizi wamebuni mbali hadi kulima jamii maalum ya nyanya isio na ladha kwa ajili tu ya tukio la mwaka. Shangwe za sikukuu zinaanza karibia saa 4 asubuhi wakati washiriki wanashindana kunyakua paja ya nyama iliokazwa juu ya nguzo yenye grisi. Watazamaji wanamwagilia maji viparaganyio wakati wanaimba na kucheza mitaani. Wakati kengele ya kanisa inagonga saa sita mchana, lori iliyopakizwa nyanya inapita ndani ya jiji, wakati nyimbo ya "To-ma-te, to-ma-te!" inafikia kilele. Tena, na mashambulizi ya mzinga wa maji, tukio kuu linaanza. Ni ule mwanga wa kijani wa maangamizi na kutupa nyanya kwa jitihada zote ya shambulio dhidi ya washirika wenzi. Warusha-nyanya kwa mbali, wauaji walenga-kwa-karibu, na wenye shabaha ya wastani wanapiga makombora. Hata ufundi wako uweje, wakati ukifika ukingoni, utaonekana (na kuhisi) tofauti kabisa. Karibu saa moja baadaye, watupaji mabomu waliolowanishwa na nyanya wanaachwa wacheze ndani ya bahari laini na chepechepe ya mtaa salsa na mabaki ndogo inafanana nyanya moja kupatikana. Mlio wa pili wa mzinga unaadhimisha mwisho wa mapambano. | Entry #19021 — Discuss 0 — Variant: Not specified
|